Thursday, 1 August 2013

VITABU VYA MWANDISHI.

VITABU  VYA MWANDISHI.

           Vitabu hivi ni adimu na havipatikani kwa urahisi kwani havijaenea kila mahali duniani. Ni neema ya pekee kuwa na nakala ya vitabu hivi, kwani vitakuwa msaada wa kiroho kwako binafsi ndugu, jamaa, majirani, marafiki, wapenzi, wafanyakazi, watumishi na wengineo utakaowiwa  kuwapatia  zawadi hii muhimu  kwa ajili ya  maisha ya ufalme wa  Mungu.  Mungu amekusudia  kuwapa mafundisho  haya kupitia mimi na wewe ili tuweze kuwafikia  wengine kwa lugha zao na  kwa kutumia  njia mbalimbali za mawasiliano kama  tepurekoda, santuri, mikanda ya video , Redio,  Runinga, nakadhalika. Huduma  hii ya kiroho  ni ya kila asikiaye na kuamini .

1, Jinsi Mungu anavyoweza kunifunua kwa watu kwa njia (10) Hatua saba za kusikia sauti ya Mungu waziwazi-Live.Kimekuwa msaada kwa wengi kwani Mungu amejifunua na kusema nao moja kwa moja kwa kunyoosha mkono wake, kujibu maswali yao waliokuwa wakijiuliza yaliyohitaji majibu. Yawezekana kila mmoja wetu ana kiu na anahitaji kufunuliwa na kusema naye waziwazi. Jibu la kiu tulizonazo ni kupitia haya, atajibu haja zako ambazo huenda umeziomba kwa muda mrefu. Tumia hatua saba za matendo ili ajifunue kwako

2. Jifunze kusamehe na kusahau Mungu akukumbuke Kabla na Baada ya kufa na Akufunulie, “Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu). Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao”(1Kor.2:9) 

 Kitabu hiki kimekuwa msaada kwa wengi kuondoa chuki kati yao na kuchochea upendo, kubadili huzuni kuwa furaha, mauti kuwa uzima, uadui kuwa urafiki, uponyaji na mambo sawa nayo (1Kor.2:9). Baada ya Yesu kujifunua na uungu wake kuthibitisha neno. Ninaamini nawe ni zamu yako sasa upate ufunuo wa ajabu utakaokupelekea kujisahihisha na kuwasamehe wengine. Kimekuwa msaada kwa ajili ya kanisa lake pia, ili lisiwe na mawaa katika kueneza pendo lake na kumdhihirisha Mungu wa mapendo.


3. Utoaji wa sadaka matoleo aina 7 unavyoweza kusababisha Mungu Akukumbuke na Akufunulie, “Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu). Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao” (1Kor.2:9).
 Kinaachilia ufunuo wa tafsiri za utoaji wa matoleo, kwani kutoa ni zaidi ya fedha na mali, kukufunulia nguvu uungu, uweza uliositirika katika kila aina ya matoleo au sadaka unayoachilia. Matoleo hufafanya mambo ambayo huwezi kuyapata kwa njia nyingine yoyote ile. Hivyo jibu la hitaji lako yawezekana limefichwa ndani ya matoleo ya aina mojawapo kati ya saba. Wenzetu walipofunuliwa hayo yanayotaka ufahamu walikuwa wanatoa wakijua mbegu hiyo ndani yake imebeba nini? Uungu wa mtoto, kuondoa utasa, ulinzi na Baraka.


4. Kanuni saba (7) za jinsi ya kutoa sadaka/ matoleo yako yapokelewe mbinguni ili Mungu aweze kukujibu, Akukumbuke na Akufunulie… Kinajibu kwa nini wengi wanatoa (wanapanda mbegu) lakini hawavuni?. Wakati mwingine wanakuwa makini kutoa kidogo au hudhubutu kutotoa. Maana kwao hudhani kuwa  ni njia ya kupungukiwa na sio njia ya kuongeza mtaji, mafanikio, baraka na uungu. Utaelewa jinsi ya kutoa kwa ukimya  namna Mungu anavyotaka na kama alivyofanya kwa wenzetu walivyokuwa wanaambatanisha maombi yao na imani na matoleo atajibu; vivyo hivyo atatenda  kwako. Kwa kuzingatia kanuni hizo saba (7) mbingu hupokea matoleo yako.

KITABU

5. Upendo wa Agape unavyoweza kusababisha utembee na uso wakeNini maana ya upendo wa Agape, Mambo saba (7) Mungu anayatumia kama kipimo cha kuonesha unampenda hivyo, ili akukumbuke na ajifunue kwako utembee na uso na uwepo wake

6. Usikate tamaa upinzani hauwezi kuzui ahadi na Mafanikio ya Mungu kwenye maisha Utaelewa maana ya upinzani maadamu unaishi chini ya jua na kama kuna mafanikio yanayotaka kukujilia huwezi kuepuka upinzani kwani ni sehemu ya maisha,hivyo huweza kukutokea ghafla. Utaelewa mambo saba (7) ya kufanya unapotokea, ili uushinde. Wengine hawakuweza kuepuka na kupata maumivu, kushindwa na kukata tamaa. Kumbuka lengo la wapinzani ushindwe, wao wafanikiwe. Na lengo la Mungu ni uushinde, ufikie mafanikio hata hata kama wapinzani hawataki. Ukielewa vizuri itakuwa ngazi yako ya kupandia. Pia utaelewa mbinu wanazotumia wapinzani kukukwamisha. Kitabu hiki kitakusaidia uvuke hatua hiyo salama na kuongeza baraka.


7.  Jifunze Mambo 7 yatakayokusaidia Usife Haraka Kabla hujaweka Historia.Kitabu hiki Kinajibu maswali mengi kuhusu kifo kama, kwa nini watu wanakufa haraka? utaelewa Sio mpango wa Mungu ufe haraka na  utaelewa vitu vinavyoua maisha na kujihadhari navyo; wakiwemo rafiki zako ndiyo wanaosababisha au kuwa ni adui zako. Jifunze kuwa urafiki ni kama kusoma kitabu, kuwa Makini nao. Hivyo utaelewa jinsi ya kuzuia kifo. Maisha yako ni muhimu kwako na sio kwa wengine Mungu, wazazi na wewe ndiyo tu hujua thamani yake.

© Cleopa E.  Soi
    Ambassador of Jesus in Tanzania   

 (Balozi wa Yesu Tanzania)    

Mob: +255753-388006, +255715-579580, +255768-759910.   

 Email: cleopaesoi@gmail.com, cleopasoi@yahoo.com.    http://baloziwayesutanzania.blogspot.com

             Vitabu hiki vinalindwa na sheria za haki miliki  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo hauruhusiwi kuchapisha, kunakili, kudurufu na kurekodi kwa njia yoyote ile bila idhini ya  mwandishi. Wala kutafsiri katika lugha yoyote ile. Hatua kali zitachukuliwa kwa atakayebainika.

SHUKURANI Ni imani yangu, Mungu ataweka jambo jipya ndani yako ambalo sio rahisi kufutika wala kufutwa na shetani au mtu yeyote. Kwani Yesu alinena “juu ya mwamba huo nitalijenga kanisa langu” wala milango ya kuzimu haitalishinda. Alivyobadilisha taifa lake wakati ule kupitia mafundisho ya namna hii , kufungua macho na ufahamu wako wa kiroho na macho ya mioyo kuyatia nuru umwone Mungu katika yale ambayo  unamtarajia zaidi; Maana.“Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda” (Yohana13:17) Ashukuriwe Mungu katika Kristo Yesu pamoja na Roho wake Mtakatifu.Tu mashaidi pamoja na wote; waliotafakari mafundisho haya kwamba yamekuwa baraka kwa kila aliyesoma na kuyatafakari.  Tunaamini nawe utaungana nasi na waliofanya hivyo kuamini sio sisi bali ni Kristo Yesu. Kuchukua  hatua kumwinua, kumtukuza,  kumpa sifa na utukufu wote kwa ufunuo  na kwa neema yake kuamua kuachilia ukuu, uweza, enzi, ubora, mamlaka na usultani, utajiri, heshima na kushinda kwa ajili yako katika kusamehe, 

“Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu, naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina! (Efeso3:20-21)“…BWANA ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu ameniita jina langu. Naye anifanya kichwa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake amenisitiri, naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo lake amenificha...
Na sasa BWANA asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake ... (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya BWANA, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu);. ... yeye aliyedharauliwa na wanadamu; yeye anayechukiwa na taifa hili; yeye aliye mtumishi wao watawalao;... BWANA aliye mwaminifu,
    Mtakatifu wa Israel aliyekuchagua. BWANA asema hivi, Wakati uliokubalika nimekujibu, na siku ya wokovu nimekusaidia; nami nitakuhifadhi, nitakutoa uwe agano la watu hawa, ili kuinua nchi hii, na kuwarithisha urithi uliokuwa ukiwa; kuwaambia waliofungwa, Haya,tokeni; na hao walio katika giza, Jionyesheni ... kwa maana yeye aliewarehemu atawatangulia, naam, karibu na chemchemi za maji atawaongoza.”(Isa49:1-10)

Maombi, “Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu; Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo. Na hata nikiwa mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, na kila atakayekuja uweza wako. Na haki yako Ee Mungu, Imefika juu sana. Wewe uliyefanya mambo makuu; Ee Mungu ni nani aliye kama Wewe?” (Zaburi71: 17-19)

No comments:

Post a Comment